top of page

COMMUNIQUÉS DE PRESSE

CongoRiver

Déclaration politique du 30 novembre 2015

Updated: Jan 25, 2021


Kwa jina la chama chetu cha kisiasa kinacho wakilisha jamii ya wakongomani hapa inchini Marekani (U.S Congolese Community) The Party of Democrats for the Development of Congo (P.D.D.CO), tunapongeza juudi za jumuiya ya kimataifa, Marekani kwa upeke, na zile za ukanda zinazo saidiya kwa hali moja au nyingine. kupatikana kwa amani inchini mwetu DRC, Ni zahiri kwamba inchi yetu ina matatizo mengi ya kisiasa, hali ambayo imesababisha mipasuko katika vyama vya kile kinacho itwa upinzani, na vile vinavyo muunga mkono rais joseph Kabila na chama chake cha PPRD. Hali hiyo imewafanya wananchi, kutokuelewa wapi inchi yetu inapoelekezwa na wale wanaoitwa wafanya siasa pande zote mbili, kama tunavyozitaja hapo awali.


Matatizo ya kiutu na kijamii pamoja na ukosefu wa amani na usalama, hasa katika mashariki ya Congo (DRC) vimesababisha utata (Confusion) miongoni mwa wafanya siasa, huku wale wa upinzani wakimchota vidole rais Joseph Kabila kwamba yeye ndiye ameharibu inchi, ameshindwa kuleta maendeleo, kwa lugha ya mabadiliko (changement) kama vile wanainchi walivyotarajia kuyaona chini ya uongozi wake.


Shutuma nyingi za wanainchi kwa upande wa serekali zimewafanya hata waliokuwa wa shirika wa karibu wa rais Joseph Kabila kumkana na kumkimbia, huku wakijipanga katika makundi mapya ya upinzani wa kiwa wakitowa madai ya sio na ukweli kwake Rais Joseph Kabila, kwa kumutopia makosa yote hata kuyasahau mazuri alio wafanyia wananchi. watu hao wanatumia mbinu za kuwandanganya wanainchi wa Congo kwa kutaka kuwachukuwa mateka kisaikolojia ili kuweza kujipanga upya kwa malengo ya kupata nafasi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika inchini mwaka 2016.


Watu hao wenyewe ndio waliosababisha utata katika swala nzima la uongozi bora wa nchi (Bonne Governance), huku wakidanganya wanainchi kwamba rais Joseph Kabila anataka kugombea tena muhula wa tatu, madai ambayo hayana ukweli. Ndugu zangu wanainchi wa Congo, watu hao hawana sababu za kuwadanganya kwa maana wao hao ndio waliosababisha hayo yote mazara ya kisiasa na kiuchumi inchini mwetu. Ni lazima kuelewa kwamba Rais Joseph Kabila asingeweza kuharibu inchi peke yake na vile vile rais asingeweza kuleta mabadiliko peke yake. Ikiwa upo uharibifu uliofanyika ni wao hao ndio waliokua watekelezaji wakubwa wa mpango huo, kwa hiyo hawana sababu za kumlaumu rais Joseph Kabila.


Kulingana na hali ilivyo kwa sasa inchini inaomba juudi za haraka kufanyika ili kuikowa inchi yetu isidumbukia katika wimbi la machafuko na maangamizi, kwa hiyo ni jukumu la kila m’moja kuona kwamba suluhisho la matatizo ya Congo laweza kupatikana kwa pamoja na sio kwa mtu m’moja, au kundi fulani la kisiasa kwa maana ni wazi kwamba kwa pamoja tunaweza kuijenga Congo mpya yenye nguvu mpya na mwelekeo mpya wa maisha ya wanainchi na vile vile mwelekeo mpya wakisiasa, hata kuweza kuzifuta aibu zote walizo nazo wanainchi wa Congo mbele za mataifa (concert des nations).


Hutuba za hao waliojiuzuru serikalini kwa madai kwamba rais Joseph Kabila ameshindwa kuiongoza inchi ni upuuzi mkubwa, kwa maana kujiuzuru kwao ndiko kunaoshuhudia kushindwa kwao na hawafai katika ujenzi wa taifa, ni mabepari wa kisiasa ambao mipango na malengo ya kuendelea kuwaiba na kuwanyonya wanainchi imekwamishwa na rais Joseph Kabila.


Ndugu wanainchi wapendwa, ni jambo njema kuelewa kwamba tangu nchi yetu ilipotoka uhuru kutoka katika makucha ya ukoloni mwaka wa 1960, bwana Joseph Kabila ndiye Rais wa kwanza kuifikisha nchi yetu katika uchaguzi huru, na wa kidemokrasia kwa maana ya chaguzi za vyama vingi, na kuifanya inchi yetu kuandika ukurasa mpya wa kihistoria. Kwa hiyo, ni tendo la kujivunia kwetu mbele za mataifa, na linaloshuhudia ukuwaji wa democrasia changa inchi mwetu, baada ya kuangusha kuta za utawala wa udikteta wa miaka thelathini na wawili (32 years) hiyo nisura mpya ambayo rais Joseph Kabila ameipa inchi yetu ya DRC.


Ni historia nzuri ambayo haitafutwa katika vizazi vya enzi za leo, na vile vya enzi zijazo katika inchi yetu, kwa hiyo Rais Joseph Kabila ni muasisi wa demokrasia iliyokua hadisi inchini mwetu. Ni lazima demokrasia hiyo changa iendelee kulindwa na kukuzwa kwa faida ya walio wengi, baada ya kurudishwa nyuma na kudidimizwa kwa faida ya walio wachache wenye chenga za mbegu za ubepari.


Ni wajibu wa kila mkongomani kuelewa kwamba, ubepari, ukoloni, na ukoloni mambo leo ni mambo yamepitwa na wakati katika ulimwengu wetu wa kisasa, ambao ni wa utandawazi (Globalization), lazima demokrasia kue na kuheshimiwa inchi mwetu, kwani pekee ndiyo njia ya amani, maendeleo na usalama pia na ujenzi mpya wa taifa letu.


Wakati huu wa muhula wa pili wa Rais Joseph Kabila kuelekea ukingoni ni nafasi nzuri pia na wajibu wa kila m’moja kuelekeza fikra zake katika uchaguzi wa viongozi wapya ili kuendeleza demokrasia, lakini pia kuikuza miongoni mwa wanainchi badala ya kuibomoa kwa kutumia nguvu. Kwa hiyo, hatutakosa kuonyesha wanainchi kwamba ni lazima uchaguzi kufanyika kila muhula (Mandate) uliopangiliwa kikatiba unapo fika kwenye ukomo wake, lakini pamoja na hayo ni fahari kubwa na nia nzuri ya kisiasa kwetu kuwaonyesha kwamba ni vema uchaguzi kufanyika katika mazingira ya haki, ukweli, na uwazi ili kuepuka m’momonyoko wa misingi ya demokrasia katika matokeo ya uchaguzi, pia kuilinda heshima ya inchi yetu na watu wake.


katika muono huu, ni vema kwamba unapo andaliwa uchaguzi lazima yawepo mambo ya awali ya uchaguzi kwa lugha nyingine “Préalable Electorales” kwa hiyo tunaomba:


  1. Tume ya uchaguzi kuandaa kalenda mpya ya uchaguzi , ikitanguliwa na ukaguzi wa daftari ya mpiga kura “Fichier electoral”

  2. Serekali itengeneze barabara ili kuwezesha wafanya kazi wa tume ya uchaguzi na wale wachunguzi wa kimataifa kufika maeneo yote ya Kongo bila matatizo.

  3. Kujenga mitambo ya mawasiliano inchini kote kwa mawasiliano haraka katika matangazo na ripoti za matokeo bila ya ucheleweshaji.

Basi kwa kuboresha hao yote, lazima mazungumzo ya kisiasa (Dialogue Politique) inayoitishwa na Rais Joseph Kabila ifanyike bila ya msuluhishi kutoka katika umoja wa mataifa, kwa sababu Kongo ni inchi huru na ina mamlaka ya kuongoza mambo yake yenyewe.


Katika hatuwa hizo, wafanya siasa na wanainchi wote waelewe kwamba serikali ya Kongo ni yenye madaraka halali kikatiba na inayo kubaliwa inchini DRC, Afrika na mbele za madola makubwa. Ni jambo la muhimu kuelewa kwamba lazima mazungumzo hayo yafanyike katika misingi ya kujenga, kwa hiyo ni lazima Rais Joseph Kabila aongoze dialogue kwa kuleta ufanisi wa maandalizi ya uchaguzi. Nivema wakongomani wote kuelewa kwamba matokeo mazuri ya uchaguzi yatapatikana kulingana na maandalizi mazuri. Ndugu wapendwa wakongomani, tunaitaji uchaguzi bora wala sio bora uchaguzi.


Basi, tunawaomba wanainchi wa Kongo, umoja wa Afrika, Marekani kwa upekee na jumuiya ya kimataifa kusapoti kwa hali na mali Rais Joseph Kabila kwa mpango wa dialogue politique ili inchi yetu ipate amani.


kihishi chama chetu cha PDDCO

Ihishi inchi yetu ya Kongo

Ihishi inchi ya Marekani


Kwa niaba ya PDDCO na Congolese Community

Jacques Abandelwa Kambi, President

Comments


bottom of page